Albam hii kutoka kwa Mabanati wa muuminina ilitakiwa kutoka 2023 lakini kutokana na sababu ambazo zilikua nje ya uwezo wa Uongozi wa Muuminina ndipo ikaweza kutolewa 18-2-2025 pia hapo awali ilitakiwa kutoka na kasida nne pekee ila baada ya muda kusonga mbele ndipo ikaweza kutoka na qaswida 10 na zote zikiwa na mfumo wa video
Na qaswida hizi zikiongozwa na Ukhty Aze. Pia tukiwa na ushirikiano pamoja na Aqaz Ladies pamoja na ukhty Fatma wa Tarbia Mabanati.
Kwa ambae anahitaji nakala ya albam hii basi anaweza kuipata pale kwenye ofisi za Muuminina
Au kwa kupiga simu 0774761879/0624027448


Comments
Post a Comment
Toa maoni yako