JE! UNAIFAHAMU HALI YA ALI ISMAIL KWA SASA KUHUSU MARADHI YAKE





 Msanii mkubwa wa Qaswida hapa Zanzibar Ali ismail kwa sasa anasumbuliwa na maradhi ambayo yamemfanya ashindwe kutembea.

Ali ismail anajulikana sana kwa qaswida zake kama vile 

Mkataa kwao mtumwa 

Kijungu

Kafara

Safari

Kitendawili 

Ali ismail alikua ni miongoni mwa wanafunzi bora pale Al-madrasat Qadiria Amani Zanzibar.

Ali ismail kupitia kurasa zake za tiktok ameweza kushare video inayoonesha akiomba msaada kuhusu maradhi ambayo yanamsibu kwa sasa anahitaji kigari cha kutembelea pia kwa mwenye uwezo wa fedha kuweza kumchangia.


HILI NI LETU SOTE WAPENDA SANAA YA QASWIDA LEO YEYE KESHO SISI.

Comments

Post a Comment

Toa maoni yako